Search again

Jumatatu, 25 Septemba 2017

MICHUZI TV: DC MSHAMA AWATAKA WANAOMTUKANA RAIS MITANDAONI WAACHE TABIA HIYO



SERIKALI YADHAMIRIA KUFIKISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJI VYOTE NCHI NZIMA
Serikalo ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imedhamiria kufikisha huduma za mawasiliano kwenye vijijini vyote nchi nzima na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wote,kwa wakati,uhakika na muda wote.
Hayo yameelezwa na mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga wakati wa ziara iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi.

Hali ya Ukosefu wa mawasiliano kwa nyakati za usiku imekuwa ikijitokeza kwenye baadhi ya maeneo ya vijijini ambako hakuna nishati ya uhakika ya umeme ambapo kampuni za simu zinatumia umeme wa jua kuendesha minara ili iweze kutoa mawasilliano kwa wananchi.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya miundombinu Mhe.Prof.Norman Sigalla King (wa kwanza kulia) akkifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha kweinsewa kkilichopo kata ya Nkolamo,wilaya ya korogwe vijijini mkoani Tanga wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kkukagua ujenzi wa minara na upatikanaji w ahuduma za mawasiliano kwenye vijiji.
Bibi Mwanafuraha Nyange,mkazi wa kijiji cha ziwa Jipe kilichopo kata ya Jipe wilaya ya mwanga kwenye mkoa wa Kilimanjaro akieleza ummuhimu wa mawasiliano vijijini kwa wajumbe wa kamati ya bunge ya miundombinu wakati wa ziara yao ya kukagua ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.
Mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (ucsaf) Eng.Peter Ulanga (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo mbele ya kamati ya bunge ya miundombinu na wakazi wa kijiji cha ziwa jipe kilichopo wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.Wa pili kushoto ni mwenyekiti wa kamati hiyo Prof.Norman Sigalla King.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA